Mchango Wa Kampuni

Ajira Kwa Vijana Na Wataalam

Kampuni imeajiri wafanyakazi 6 kwa wastani wengi wakiwa ni vijana ambao wamemaliza vyuo vya hapa nchini.
Pia kampuni inatoa fursa kwa wataalam mbali-mbali kama watalaam wa mpango mji, wapima ardhi, komputa (IT professionals), masoko (marketing professionals) na kadhalika.

Ushiriki Kwenye Sekta Binafsi

Kampuni ya Mrisho Consult Limited pia inachangia mambo mbali-mbali ya maendeleo ya sekta binafsi ndani na nje ya nchi.

Mchango Wa Kampuni Katika Jamii

Kutenga na kutoa bure maeneo ya taasisi za serikali mfano vituo vya polisi, ofisi za jeshi la zimamoto, maeneo ya makaburi, kuchimba visima virefu na vifupi maeneo mbalimbali ndani ya nje ya miradi ya kampuni, kusogeza huduma za nishati ya umeme ndani na nje ya maeneo ya miradi ya kampuni, kufungua barabara zinazounganisha maeneo ya jirani ya miradi na mitaa. Kufadhili na kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii mfano ujenzi wa shule, zahanati na nyumba za waalimu, shughuli za michezo mfano matamasha.

Mchango Wa Kampuni Katika Kukuza mji Mkuu wa Dodoma

Katika kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli kufikia uchumi wa kati wa viwanda, kampuni imeamua kushirikiana na kituo cha utangazaji cha Redio na Televisheni cha Clouds Media Group ili kuweza kuhamasisha wananchi waliopo ndani na nje ya nchi kwa kutangaza viwanja vya jijini Dodoma.