Mfumo Wa ufanyaji Kazi
Kampuni hushirikiana na makampuni ya upimaji na upangaji miji yaliyoidhinishwa na kutambulika na bodi za wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi i.e. NCPS na TPRB.
Kampuni hushirikiana na makampuni ya upimaji na upangaji miji yaliyoidhinishwa na kutambulika na bodi za wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi i.e. NCPS na TPRB.
Kampuni ina namna tatu za kupata maeneo ya miradi ikiwa ni baada ya kujiridhisha uhalali wa milki, mipaka na ukubwa kuanzia ngazi ya mtaa, kata na wenyeji wa asili na majirani wanaoaminika mpaka ngazi ya wilaya, mkoa na wizara. Aina hizo ni kama ifuatavyo:-
I.Kununua maeneo na kushirikiana na makampuni ya upangaji na upimaji pamoja na mamlaka za serikali (kutoa
ushauri, kusimamia na kuidhinisha) mradi;
II. Kuingia ubia na wamiliki wa asili ambapo kampuni huingiza mtaji na kugharamia shughuli za upangaji, upimaji na uwekaji miundombinu (barabara, umeme na maji –katika baadhi ya miradi); na
III. Kuingia mikataba na wadau waliopima miradi yao binafsi kwa kuwatafutia masoko na kuboresha miundombinu ili kuvutia wanunuzi kuweza kuyaendeleza kwa urahisi na haraka.
a. Kampuni inaandaa mazingira ya uendelezaji katika kuhakikisha maeneo ya mradi yanapitika kwa urahisi kipindi
chote chamwaka;
b. Kampuni ina vifaa mbalimbali vya kisasa vya upimaji ardhi na kupanga miji ambavyo vinawawezesha kampuni
shirika zilizosajiliwa katika fani hizo kuweza kufanya kazi kwa wepesi, ufanisi na haraka;
c. Kampuni hupeleka nishati ya umeme katika miradi ili kuharakisha maendeleo;
d. Kuweka madaraja/kalavati ili mawasiliano yawepo kipindi chote cha mwaka;
e. Kusogeza huduma za vifaa vya ujenzi na malighafi; na
f. Kuchimba visima katika maeneo yaliyo na mahitaji ya maji.
Baada ya kuandaa miradi, viwanja vinauzwa kupitia mfumo ufuatao:
i. Kushirikiana na halmashauri za wilaya na manispaa katika kuuza;
ii. Upendeleo maalumu wa masharti nafuu ya malipo kwa watumishi wa umma mfano waalimu, wauguzi na makundi mengine mfano waendesha bodaboda na wafanya biashara ndogondogo (wamachinga).
Katika kuvutia wawekezaji na wateja, kampuni inatumia mbinu tofauti katika matangazo, kwa mfano:
1) Kampuni imeshiriki katika maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya sabasaba kuanzia mwaka 2020;
2) Kampuni ina jarida lake la kila mwezi linalosambazwa bila kuuzwa kwa watu na ofisi mbalimbali nchini kote bara na visiwani. Jarida hili linatangaza fursa zilizopo katika miradi ya kampuni na pia taarifa na ushauri mbalimbali kuhusiana na uwekezaji katika ardhi;
3) Kampuni inachukua picha za anga na kuzisambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii na tovuti yake ili kuwafikia watu mbalimbali nje na ndani ya nchi katika kupanua soko na fursa zilizopo katika eneo husika;
4) Ushiriki wa kampuni katika kuwezesha matamasha mbalimbali ya michezo.
5) Kupitia mitandao ya kijamii; na
6) Kupitia vipeperushi.
Kampuni imebeba jukumu la kugharamia na kufuatilia mchakato wa upatikanaji wa hatimiliki kwa kumfuata mteja popote alipo ili kujaza taarifa zinazotakiwa katika mchakato wa umilikishwaji. Mfumo ambao huwarahisishia kwa wateja wanaouziwa viwanja na kampuni yetu, ambapo mpaka sasa hatimiliki takribani ishirini (20) zimeshatolewa na wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi na kupatiwa wamiliki.